Sep 22, 2016

Posted by Dismas Ten Thursday, September 22, 2016 No comments


MCHEZO wa  ligi kuu ya soka Tanzania bara kati ya Mbeya City fc na Tanzania  Prison  uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine  jijini Mbeya  umemalizika kwa  suluhu ya bila  kufungana.

Kwenye mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute, timu zote  zilishambuliana kwa zamu katika vipindi vyote viwili lakini hadi dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliyofanikiwa  kuona lango la mwenzake.

Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Kinnah Phiri kwa kuwatoa  Issa Nelson, Joseph Mahundi na Ramadhani  Chombo, na nafasi zao kuchukuliwa na Michael Kerenge, Ditram Nchimbi na Salvatory Nkulula hayakuweza kubadili matokeo ya mchezo huo uliozikutanisha timu hizi mbili hasimu.
Mara baada ya mchezo Kocha Phiri  pamoja na maneno mengine kadhaa  alisema kuwa makosa kadhaa kwenye safu ya ushambuliaji yaliinyima City ushindi kwenye mchezo huo.

“Timu imecheza vyema,tutafanyia kazi makosa kadhaa yaliyojitokeza leo kwenye safu yetu ya ushambuliaji, soka iko hivyo, ni jambo jema  tumepata pointi moja  tunaanza maandalizi ya mchezo ujao  tutakaocheza ugenini huko Mlandizi”, alisema.

Aug 21, 2013

Posted by Dismas Ten Wednesday, August 21, 2013 No comments



          Nyota wa Man U anayepewa nafasi ya kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu msimu huu

Mapema wiki iliyopita nyota wa Manchester United Mholanzi Robin Van Persie alidhihirisha Ubora wake baata ya kufunga moja ya mabao muhimu kwa timu yake katika ushindi wa Bao 4-1 dhidi ya Swansea City.

Oct 23, 2012

Posted by Dismas Ten Tuesday, October 23, 2012 No comments
 Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Oktoba 24 mwaka huu) kwa mechi nne za raundi ya tisa huku Azam ikiusaka usukani wa ligi hiyo ikiwa mwenyeji wa Ruvu Shooting.
 
Mechi hiyo namba 60 ambayo kama Azam itashinda itafikisha pointi 20, hivyo kuwa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam. Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
 
Yanga itawakaribisha Polisi Morogoro ambao ndiyo wa mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom hivi sasa katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
 
Alex Mahagi kutoka Mwanza ndiye atakayepuliza filimbi kwenye mechi hiyo namba 62. Waamuzi wasaidizi ni Frank Komba na Michael Mkongwa, wote kutoka Iringa wakati mwamuzi msaidizi ni Oden Mbaga anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wa Dar es Salaam.
 
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya African Lyon ya Dar es Salaam ambao ni wageni wa Coastal Union inayonolewa na Hemed Moroco. Nayo Mtibwa Sugar itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko kwenye mashamba ya miwa Turiani mkoani Morogoro.
 

Sep 13, 2012

Posted by Dismas Ten Thursday, September 13, 2012 No comments

Meneja masoko wa Grandmalt, Fimbo Butala (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa ZFA, Masoud Attai Masoud na Mwanasheria wa ZFA katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Zanzibar mara baada ya kukamilika kwa semina ya wanahabari kuhusu ligi kuu ya soka ya Grandmalt kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View leo.

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter