KATIKA hali ya kawaida binadamu yoyote hupenda kupata mafanikio kwenye kila jambo analokuwa analifanya niwazi kuwa unapoamua kufanya kitu kwa kushirijkiana na mtu mwingine halafu akaonekana kutokuwa mkweli katika mambo kadhaa mabayo ulikuwa umekubaliana naye basi hakuna jambo lingine la kufanya zaidi ya kuachana naye
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa msukuma kandanda maarufu wa England Sol Campbell aliyewahi kucheza soka kwenye klabu kadhaa kubwa nchini humo kama Arsenal , Potsmouth na hata timu ya taifa ya nchi hiyo (The Three Lions)
Baada ya kuachana na Potsmouth Campbell alikwenda kujiunga na timu ya daraja la 4 Notts County kwa mkataba wa miaka 4 na kukutana kocha wa zamani wa England Sven Goran Erickson lakini mara hii akiwa ndiye mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo inayojipanga kupanda daraja ili iweze kucheza Premier League
Kabla Campbell hajakubari kusaini mkataba huo kulikuwa na makubariano maalum na viongozi wa Timu hiyo ikiwa ni pamoja na ahadi kubwa za kuiboresha timu kwa kufanya usajiri mzuri ili iwe na kikosi kikali kitachokuwa kikipigana kuipandisha timu hiyo
Lakini mpaka timu inaingia uwanja kuanza michuano ligi daraja la 4 hakukuwa na kitu hata kimoja kilchotekelezwa miongoni wa makubaliano yalyokuwepo baina ya Campbell na uongozi wa timu hapo ndipo nyota huyo alipoona kuwa viongozi hao wamemdanganya na baada yta kumalizika kwa mchezo hakuwa nasababau nyingine ya kusubiri zaidi ya kuchukua kilicho chake na kuwaaga wachgezaji wenzake na kisha kutimua zake.
Ni uamuzi ambao uliwashangaza na kuwashituwa wengi akiwemo Sven Erickson lakini nyota wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amekaririrwa na gazeti moja la michezo nchini humo akisifia uamuzi aliouchukua Campbell na kuongeza kuwa hata kamaangekuwa yeye angafanya hivyo kwa kumdanya mchezaji mkubwa kama Campbell ni kumdhalilisha
Muda mfupi baada ya kuikacha Notts Caunty tayari klabu kadhaa zimetangaza kumpa ofa ya usajiri wakati wa dirirsha dogo mwezi januari ikiwemo timu machacha ri ya Hull City,Ipswch Town,West Ham United,Fulham na Totteham Hotspurs
Sakata hili la Campbell linaweza kuwa somo tosha kwa wachezaji wa Tanzania ambao wako radhi kumaliza soka lao wakiwa bechi kwenye timu za Yanga na Simba kutokana na kukubari ahadi hewa wanazopewa na viongozi wa timu hizo wakati wa usajiri na mwisho wa siku wanabaki na sifa ya kuwa kwenye vilabu hivyo nabaadae wanaachwa wakiwa hawana mbele wala nyuma
Wapo wachezaji wengi amabao kabala ya kujiunga na timu hizo walikuwa wanogopwa kutokana na uwezo wao uwanjani miongoni mwao ni Primus Kasonso,Osward Morris, amabao walikimbia ajira zao wakati wakiwa kwenye kiwango cha juu na kuicha Prisons na kukimbilia hadi hewa lakini muda mfupi tu wamepotea
Lakini kama wangekuwa makini na kuutambua mustakali wao mpaka leo nyota hao wangekuwa bado wanauwezo mkubwa uwanjani na kula matunda ya soka la bongo hivi sasa linalozidi kuchanua kila kuchapo.
Kuheshimu mawazo yao pengine ni jambo ambalo limekuwa mzigo mkuwa kwa wanasoka wa hapa na kujikuta wanakubari kirahisi kuingia kwenye mitego ya timu hizo zenye sifa ya timu kubwa pasipo kuwa na mipango mathubuti ya maendeleo ya klabu zenyewe ama wachezaji ambao kwa namaa moja ama nyingine wanaweza kabisa kucheza mpira muda mrefu wakiwa nje ya timu hizo mfano mzuri ukiwa kwa nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Macky Maxime.
0 COMMENTS:
Post a Comment