Jul 29, 2010

Posted by Dismas Ten in | Thursday, July 29, 2010 No comments

Mwanamitindo maarufu nchini Marekani Christine Mendoza amesema ameandaa mpango maalumu wa kumnasa kimapenzi nahodha wa wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry aliyejiunga na timu ya New York Red Bulls inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo ‘MLS’ hivi karibuni

Habari kutoka mtandao mmoja wa mastaa huko ‘mbele mbele’ zinadai kuwa Mendoza aliwahi kulifukizia bila mafanikio penzi la mwanandinga huyo msimu uliopita alipokuwa nchini humo kwa mapumziko kipindi cha majira ya joto.

“Watu wengi wanazungumza juu ya kile nilichokifanya mwaka jana, lakini kwangu ni tofauti safari hii nimejipanga kumnasa Henry kwa gharama yoyote sababu nampenda na nina imani wakati huu itakuwa rahisi zaidi kwa sababu sasa atakuwa hapa muda mwingi” alisema

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter