Dec 2, 2009

Posted by Dismas Ten in | Wednesday, December 02, 2009 No comments

Katika hali ya kushangaza, mapema wiki hii Mwanamitindo mahiri nchini Ureno, Nereida Gallardo amewaambia waandishi wa habari kuwa, hatasahau kamwe maishani mwake siku ambayo alipata nafasi ya kujirusha na msukuma kandanda maarufu wa nchi hiyo Christiano Ronaldo ambaye kwa sasa anasukuma gozi kunako klabu ya Real Madrid ya Uhipania,

Habari zilizopatikana kwenye mtandao mmoja nchini humo zinasema kuwa, licha ya kutemwa katika mazingira ya ajabu na msukuma kandanda huyo, Nereida bado hana kinyongo naye na aliongeza kwamba, daima atamkumbuka na kama ikitokea atamuita tena kwa ajili ya mapenzi atafanya hivyo haraka bila kujali yuko upande gani wa dunia.

‘Siku hiyo baada ya kumalizika kwa zoezi la kupeana mapenzi moto moto, nililazimika kuwaomba wamiliki wa hoteli tuliyokuwa tumelala ili wakubali kuniuzia vitu vyote tulivyotumia ikiwa ni pamoja na mashuka na taulo ambazo mpaka leo hii nimevihifadhi vizuri kwenye moja ya makati yangu nyumbani na vitabaki kama kumbukumbu yangu muhimu.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter