Jul 20, 2010

Posted by Dismas Ten in | Tuesday, July 20, 2010 No comments

Namshukuru Mungu kwa kunipa uhai mpaka simu ya leo na kunifanya nipate kuongea nawe msomaji kwa njia hii ya safu ya mkasa wa simu.

Kwa jina naitwa Zairuni Mohamed nina umri wa miaka 25, nipo Nyakamwaga wilaya ya Geita, mkoani Geita. Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa safu hii ambayo imekuwa ikisomwa na watu wengi kutokana na kila mmoja kuwa na fursa ya kusimulia mkasa wake bila tashiwishi yoyote.

Leo nami nimelazimika kuusimlia mkasa wangu huu wa kweli ambao ulinipata na baada ya kukuchati na mwanaume nisiyemfahamu kwa muda mrefu lengo likiwa ni siku moja tume mume na mke.

Mimi ni mpenzi mzuri sana wa magazeti ya Kiswahili. Siku moja nilipata namba kwenye gazeti ya mwanaume aliyejitambulisha kuwa ni Ally Hassan mkazi wa Dar es Salaam ambaye alikuwa anatafuta msichana wa kuoa.

Nilifurahi kupata namba hiyo kwani nami nilikuwa nasaka mwanaume wa kunioa mwenye sifa ambazo ninazo zipenda. Nilipoipata namba hiyo nilimtumia sms ya kujitambulisha kwake naye bila hiyana alifanya hivyo na ndiyo ukawa mwanzo wa mahusino yetu ya kimapenzi.

Tulianza kutumiana sms kila itwapo leo na wakati mwingine nilikuwa naona usumbufu kufanya kazi nyingine badala ya kuchati na mpenzi wangu huyo.

Cha ajabu kila sms yake aliyokuwa anaituma ilikuwa inausisimua sana mwili wangu na kunifanya kuwa na shauku ya kufanya tendo la ndoa. Lakini ilishindikana kufanya hivyo kutokana na kukosa bwana wakufanya naye mchezo huo kwani anayenifanya niwe na hali hiyo yupo Dar.

Hali hiyo iliendelea kinitokea kwa muda mrefu na kunifanya kuwa mtumwa wa mapenzi kwani, muda mwingi niliutumia kumuwaza yeye na sikuwa na chembe hata kidogo ya kutafuta mwanaume mwingi wa kumaliza haja yangu.

Kwa kipindi cha miezi mitatu alikuwa anachati mchana, lakini baada ya muda Ally alibadili muda na kuanza kufanya hivyo usiku. Nilimuomba tukutane ili tufahamiane lakini yeye alisema bado ana shughuli anazozifanya wakati ukifika atanitafuta.

Kitendo cha kukubali kuchati usiku na Ally kulinifanya niwe mgonjwa zaidi katika hisia za mapenzi kwani kila sms aliyokuwa anaituma ilikuwa inanichanganya kutokana na mpangilio wake wa maneno matamu.

Mara nilianza kuota ndoto nikiwa nafanya tendo la ndoa na mwanaume kwa hisia zisizo kifani. Hata hivyo ndoto hizo zilionekana kuwa ni zakweli kwa sababu nilipokuwa nashtuka usingizini nilijiona tayari nimesha maliza haja yangu ya tendo la ndoa.

Sikuelewa mara moja kwanini hali hiyo ilikuwa inanipata, kwani mbali na kuona nimemaliza haja ya tendo la ndoa, mwili wangu pia ulikuwa mchovu kiasi kwamba siku ya tukio sikuwa na nguvu ya kufanya kazi.

Kutokana na hali hiyo, nilimweleza mpenzi wangu atafute angalau siku moja aje nyumbani ama anielekeze alipo ili nimfuate nikakidhi haja yangu lakini yeye alisema kuwa, nisiwe na shaka kwani nyakati za usiku huwa anakuja na kufanya naye tendo hilo.

Kauli hiyo ilinishtua kidogo na kumwambia mbona mimi huwa simuoni chumbani kama kweli huwa anakuja nyumbani kufanya nani tendo la ndoa wakati simuoni.

Aliniambia nisiwe na haraka, ipo siku ataamini kama kweli huwa anakuja chumbani kulala na mimi. Siku moja nikiwa sina hili wala lile, alinipigia simu na kuniambia kuwa usiku nitakuwa naye hivyo nikae mkao wa kukata kiu ya mapenzi ambayo imekuwa ikinisumbua mara kwa mara.

Baada ya kuniambia hivyo, nilimwambia itakuwa vizuri tukaonana kwanza kabla ya kufanya tendo hilo kwani ni vema kuonana mapema na kila mmoja kumuona mwenzake jinsi alivyo.

Cha ajabu yeye alisema ananifahamu vema na kuanza kunielezea jinsi nilivyo ikiwa ni pamoja na mazingira ya chumbani kwangu pamoja na kitanda ninacholalia. Kana kwamba hiyo haitoshi, wakati nazungumza naye alinitajia rangi ya nguo yangu ya ndani niliyokuwa nimeivaa siku hiyo.

Maneno hayo yalinifanya nishindwe kumuelewa hasa baada ya kung’ang’ania kuwa usiku lazima aje. Kauli hiyo ilinitia uoga na kunifanya kuhama chumba na kwenda kulala na wadogo zangu sehemu nyingine. Hata hivyo suala hilo lilibaki kuwa siri yangu.

Usiku wa manane nikiwa usingizini, niliona ninatembea na mwanaume mmoja mrembo sana na kujitambulisha kuwa yeye ni Ally Hassani na kunitaka twende tukalale chumbani kwangu.

Binafsi nilionekana kuwa na furaha isiyokifani na kwenda moja kwa moja chumbani kwangu na tulipofika alianza kunishika shika ikiwa ni hatua za mwanzo za maandalizi ya tendo la ndoa.

Kila sehemu ya mwili aliyonigusa ilinifanya nijisikie nikiwa sayari nyingine, mara nilijikuta nimezama kwenye mapenzi na kuanza kula raha za dunia. Nilifanya tendo hilo kwa raha zangu bila kujua kuwa nilikuwa ndotoni.

Ghafla nilishtuka nikiwa chumbani kwangu huku kibatali kikiwa kinawaka na kitandani nilikuwa na mwanaume nisiyemjua akiwa amenikumbatia. Nilitaka kupiga kelele za kuvamiwa lakini alinikataza na kusema kuwa yeye ni Ally amekuja kukidhi haja ya maisha yangu.

Nilianza kuvuta kumbukumbu kuwa, mbona wakati nalala nilienda chumba cha wadogo zangu, sasa kwenye kitanda changu nimefikaje? Ghafla Ally alitoweka nakunifanya nipoteze fahamu, wakati anaondoka aliniambia nisimwambie mtu yeyote juu ya kilecho tokea.

Kulipopambazuka nilikuwa mtu mwenye hofu kubwa na kuamua kuifuta namba ya simu ya Ally lakini cha ajabu wakati naifuta, jumbe mfupi wa maneno uliingia ukisema “Kufuta namba yangu ya simu si dawa ya mimi kuachana na wewe, kinacho endelea naomba usimwambia mtu yeyote, ukikaidi maneno yangu, hakika utakufa.”

Mpaka leo mwenzenu bado nateswa na jinni hili ambali nililipata kupitia namba za kutafuta wachumba kwa njia ya magazeti.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter