Jul 20, 2010

Posted by Dismas Ten in | Tuesday, July 20, 2010 No comments

Naitwa Abasi, umri wangu ni miaka 22. Nina mpenzi wangu ambaye ninampenda sana lakini yeye haoneshi kama ananipenda pamoja na kuwa naye kwa muda wa miaka 3. Yeye kwa sasa ni mwanafunzi, namlipia ada ya shule na hivi karibuni nimemnunulia simu ya mkononi kwa lengo la kuwasiliana lakini cha ajabu nisipompigia mimi, inaweza kuisha wiki sijaongea naye. Siku akiwa na shida na hela hushinda akibipu kutwa nzima, naomba ushauri wako Anko, nifanyeje?

JIBU

Pole sana Anko kwa maumivu unayoyapata, kwani naelewa vema jinsi mtu anavyoumia pindi anapompenda asiyependeka. Bahati mbaya Anko hujaniambia mpenzi wako ana umri gani. Inawezekana ikawa ni suala la umri wake kuwa mdogo na bado haujaruhusu mambo ya mapenzi, ama familia anayoishi huwa inampa vitisho vya kufanya mapenzi akiwa na umri mdogo.

Hujaniambia pia kama umeshawahi kufanya naye tendo la ndoa. Kwa mantiki hiyo, nashindwa kujua tatizo liko wapi kwani endapo ningefahamu umri wake ningekupa jibu sahihi la nini cha kufanya. Pengine nisema kuwa, msichana anaweza kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kutokana na kukutana na mwanaume mwenye maumbile makubwa kuliko yeye ambayo humpa shinda wakati wa kula raha ya dunia.

Endapo msichana anapata maumivu wakati wa kufanya tendo hilo, huwa anajisikia vibaya pindi anapofikiria kukutana na mwenzi wake. Hali hiyo mara nyingi huwa inaondoa upendo wa msichana huyo kwa mwenzi wake kwa kumuona kama ni adui wake wakati wa faragha yao. Hivyo Anko naomba nitwangie simu ili tuongee zaidi na huenda nikabaini tatizo lipo wapi.

===============

Mpenzi wangu ninapomhisi anamsichana mwingine huwa mkali, nifanyeje?

SWALI

Naitwa Leah miaka 21. Ninampenzi wangu ambaye tuna malengo ya kuwa mume na mke siku za usoni na kishanitambulisha kwa wazazi wake. Lakini simuelewi ni mtu anayependa kunifuatilia kwenye mienendo yangu, ninapomhisi kuwa anamsichana mwingine zaidi yangu na kisha nikamwambia huwa mkali kama mbogo. Kihistoria ni mvulana aliyekuwa na wasichana wengi. Je, kunifuatilia kwake huku ni kuonesha kwamba ananipenda? Naomba ushauri Anko.

JIBU

Pole sana Anko Leah. Mara nyingi wanaume wenye huruka ya kuwasaliti wapenzi wao huwa wakali pindi wanapoambiwa ukweli lengo kuu ikiwa ni kujihami na kumfanya mpenzi wake asiendelee kumfuatilia ili asimtibulie raha zake. Wanaume wenye tabia hiyo hufanya vivyo hivyo pindi wanapokuwa ndani ya ndoa zao kwani dalili ya mvua ni mawingu.

Ukiona mwanaume anakuwa na idadi kubwa ya wasichana tambua kuwa huwa haliziki na mpenzi mmoja, hivyo suala la kuisaliti ndoa yake si tatizo kwake. Kwa mantiki hiyo unapoamua kuolewa na mwanaume huyo ingia ndani ya ndoa ukitambua kwamba suala la mumeo kuwa na nyumba ndogo si la kuuliza, kwani hawezi kulizika na wewe hata kama utamlizisha vipi.

Kuhusu kukufuatilia sana, hapa hakumanishi kama anakupenda bali anahisi na wewe unamsaliti, kwani wanaume wenye tabia ya uzinzi huwa wanawivu wa ajabu kwa wapenzi wao. Kinachomsumbua mchumba wako ni wivu wa mapenzi ili usimusaliti na si kwamba anakupenda.

Anko, umri wako unaruhusu kuachana na mwanaume huyo na kuangalia mwelekeo mwingine, usikubali kuingia kwenye kifungo cha ndoa chenye majuto ambayo utakuja kujuta siku zijazo ikiwa ni pamoja na kuambulia magonjwa ya zinaa. Kumbuka uchumba si ndoa, natambua pia kumuacha unayempenda kunakazi. Lakini ni heri siku zijazo ukaishi kwa raha kwenye ndoa yako kuliko kusema ungejua usingeolewa na mwanaume huyo.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter