Jul 17, 2010

Posted by Dismas Ten in | Saturday, July 17, 2010 No comments
MENEJA Mkuu Msaidizi wa Bendi ya muziki wa dansi nchini Diamond Musica International ‘Vijana Classic’, Parfect Kagisa a.k.a Pi.Diddy amedai kuwa bendi yake inahujumiwa na watu wasioitakia mema na ili kuidhoofisha wameamua kuwaua viongozi wake kwa kutumia sumu kama ilivyotokea kwake hivi karibuni.

Akizungumza na safu hii hivi karibuni jijini Dar, P.Diddy alisema kuwa kitendo cha bendi yake kuja juu na kuwa tishio kwa nyingine kimeonekana kero kwa wasioitakia mema na njia rahisi wameamua kuwatafuta kwa kuwawekea sumu kwenye chakula.

“Kitendo cha bendi yetu kufanya vizuri na kukubalika na watu wengi kila pembe ya nchi kumeonekana kuwakera maadui zetu na wameamua kufanya hujuma kwa kutuwekea sumu kama ilivyotokea kwangu hivi karibuni mpaka nikalazwa hosipitali ya TMJ,” alisema P.Diddy.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter