Jul 17, 2010

Posted by Dismas Ten in | Saturday, July 17, 2010 No comments

Mkongwe wa muziki wa dansi nchini ambaye sasa amegeukia miondoko ya kumtukuza Mungu, Ramadhani Mtoro Ongala a.k.a Dk. Remmy kwa mara nyingine Agosti 6 mwaka huu anatarajia kudhihirisha mbele ya kadamnasi kuwa yupo fiti atakapopanda jukwaani kuimba vibao vyake kadhaa wakati wa uzinduzi wa albamu ya Jua la Haki ya muimbaji wa muziki huo Joyce John Mwaikofu.

Akipiga stori na gazeti hili juzi kati jijini Dar, Joyce alisema kuwa, hali ya mwanamuziki huyo imeimalika na ili kudhihirisha hilo, siku ya event ya uzinduzi wa albamu yake Dk. Remy atasimama jukwaani na kugonga ngoma zake kadhaa kabla ya kuwapisha waimbaji wengine kama Ado Novemba, Ambene Mwasonge, Stela Joel, David Robert na Papa David Lutumba

“Siku ya uzinduzi wa albamu yangu ya Jua la haki, mkongwe wa muziki nchini Dk. Remy atapanda jukwaa ili kuidhihirishia kadamnasi itakayofika hapo kuwa yeye yupo fina na ishu hiyo itachukua nafasi kwenye uwanja wa kanisa la EAGT Kipunguni B Maji machafu Ukonga mara baada ya ibada mchana,” alisema Joyce.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter