Jul 17, 2010

Posted by Dismas Ten in | Saturday, July 17, 2010 No comments
Rankim Ramadhani.
Dj mwenye taito kubwa jijini Dar, Rankim Ramadhani amefanya kioja kisichotarajiwa na watu wengi baada ya kusimama juu ya meza na kuvunja sahani iliyojaa chipsi kuashiria kufunguliwa kwa disco na burudani atakayokuwa anaitoka kila wiki ndani ya Ukumbi wa Le Club Shengen. Tofauti na ilivyozoeleka kwenye sherehe zingine ambazo hufunguliwa kwa uzibuaji wa ‘Shampeini’, Rankim alizima ghafla muziki na kufanya kioja hicho kwa madai kuwa ni kubadili staili ya ufunguzi wa budurani hiyo. “Jamani eee naivunja sahani hii kuashiria uzinduzi wa disco na burudani za kila ‘wikiendi’ katika ukumbi huu hatuna lazima ya kutafuta ‘Shampeini’ sisi ni wabongo na mambo yetu yanakwenda kibongo bongo” alisema Rankim.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter