Dec 2, 2009

Posted by Dismas Ten in | Wednesday, December 02, 2009 No comments

MWANAMUZIKI nyota wa miondoko ya pop na kipenzi cha akinadada kutoka pande za Marekani, Justin Timberlake a.k.a Handsome Boy, amewakata ngebe ‘masister du’ kibao duniani kote waliokuwa wakipigana vikumbo kuwania penzi lake baada ya kutoa kauli kuwa, hana wazo wala mpango wa kuoa kwa kwa sasa kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi ya kufanya.

Kwa mujibu wa Jarida moja maarufu la kidaku nchini humo lijulikanalo kama Ok Magazine ambalo ndilo lilichapisha taarifa hiyo, linadai kuwa, sababu nyingine inayofanya handsome Boy huyo afute wazo la kuoa, ni kuiona ndoa kama kitanzi na aliwataka wale wote waliokuwa na matumaini ya kuolewa naye wasihangaike tena.

Hata hivyo, kauli ya Timberlake imepokelewa kwa mitazomo tofauti na wanyange waliokuwa wanawania kula bata na mwanamuziki huyo, ambapo baadhi yao walionekana kumuonea huruma mpenzi wake wa sasa wa nyota huyo, mwanadada Jessica Biel ambaye kwa upande wake ameonesha nia ya kumsubiri ajipange zaidi ili waweze kutimiza ahadi yao ya kuwa mke na mume siku za usoni.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter