Dec 2, 2009

Posted by Dismas Ten in | Wednesday, December 02, 2009 No comments

Rais wa Marekani Barack Obama anapeleka wanajeshi elfu thelathini zaidi wa Marekani nchini Afghanistan ifikapo kipindi cha majira ya joto mwaka 2010, na anapanga kuanza kuwaondoa mwaka unaofuatia. Rais alielezea mkakati wake wa kushinda vita nchini Afghanistan.

Baada ya miezi kadhaa ya kutafakari, Rais Obama ametangaza mpango wake wa kupeleka wanajeshi wa ziada nchini Afghanistan. Aliuzindua mkakati wake mbele ya wanajeshi kwenye kituo cha mafunzo ya kijeshi cha West Point huko New York, Jumanne jioni huku taifa likiangalia kwenye televisheni.

Wanajeshi wa ziada wataungana na wanajeshi wa Marekani wapatao 68,000 ambao tayari wapo Afghanistan, na maelfu ya wanajeshi wa ushirika.
Rais alizungumza huku uungaji mkono wa wamarekani ukizidi kupungua kuhusu vita. Utafiti mpya wa kituo cha Gallup unaonyesha asilimia 35 pekee ya wa-Marekani wanakubaliana na mkakati wa bwana Obama juu ya vita hivyo na asilimia 55 hawakubaliani naye.

Huko West Point, bwana Obama alisema Afghanistan haijapotea, lakini imekuwa ikirudi nyuma kwa miaka kadhaa. Alisema Al-Qaida inapanga vitendo vipya vya kigaidi kutoka hifadhi zake salama katika mpaka wa Afghanistan na Pakistan, kwa msaada wa Taliban.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter