Dec 1, 2009

Posted by Dismas Ten in | Tuesday, December 01, 2009 No comments

DADA KAMWAMBUKIZA BINTI YANGU UKIMWI PART 1.

MWANDISHI KULWA MWAIBALE

“Nilipokuwa mdogo naishi na wazazi wangu, sikufikiria kama katika maisha yangu ningeweza kukumbana na mikosi kama iliyonikuta na kunifanya nipoteze furaha ya kuishi na kutamani kufa kuliko kuendelea kuishi kwenye dunia hii iliyojaa mateso, simanzi na dhiki za kila aina.
Hata hivyo, ninapomwangalia binti yangu Mary ambaye kaambukizwa ugonjwa wa ukimwi ambao hauna tiba, namuomba Mwenyezi Mungu anipe uzima ili atakapotangulia mbele za haki nimzike kuliko kutangulia mimi na kumuacha akiteseka hapa duniani.
Jambo hilo nimekuwa nikimuomba sana mola wangu kwasababu naelewa nikifa na kumuacha Mary anayeugua maradhi hayo yasiyo na tiba, atateseka sana na kwa jinsi ninavyoona baadhi ya watu wasio na huruma watamnyanyapaa sana binti yangu.
Nasema hivyo kwasababu nimeshuhudia baadhi ya wagonjwa wa Ukimwi wakifanyiwa hivyo tena wengine na baadhi ya ndugu zao wa karibu au wa damu, hilo linaniumiza sana!
Mimi ni mkazi wa mjini Arusha ambaye kwasasa nina umri wa miaka 39.Nilioa mwaka 1993 ambapo nilijaliwa kupata watoto wawili ambao ni Mary aliyeambukizwa Ukimwi na dada yangu na mdogo wake Michael.
Baada ya kufunga ndoa na mke wangu ambaye tumetengana, maisha yalikwenda vizuri sana na upendo ulitawala katika nyumba yetu na kuwavutia watu wengi wakiwemo wazazi na ndugu zetu.
Sikuwahi kufikiria kama ingekuja kutokea siku moja tungetengana na mke wangu kipenzi, niliyempenda kuliko wanawake wote chini ya jua lakini mambo yalikwenda kinyume kwani tumetengana na mama watoto wangu na hivi sasa kila mmoja anaishi kivyake.

Kwanini bwana Mjema aliachana na mke wake kipenzi? Na nini chanzo cha bintiye Mary kuambikizwa Ukimwi na shangazi yake? Usikose kufuatilia mkasa huu wa kusisimua
Kupia blog hii

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter