Leo ni siku ya Ukimwi Duniani. Shirika la Afya Ulimwenguni limetoa takwimu zinaonyesha maambukizi ya ugonjwa ukimwi yamepungua kwa asilia mia 17 kote ulimwenguni.
Hata hivyo bado maambukizi katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara yako juu. Na huku nchi nyingi za Afrika. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema watu milioni 33.4 wanaishi na virusi vya ukimwi kote duniani, kutoka milioni 33 mwaka 2007. Lakini la kutia moyo ni kwamba watu wengi wanaishi kwa muda mrefu kwa sababu ya uwezo wa kupata dawa za kupunguza maambukizi, zinazojulikana kama ARVS. Munira Muhammad alizungumza na Bruno Ghumpi, kaimu mkurugenzi mtendaji wa shirika la kiraia la kupambana na ukimwi, nchini Tanzania, WAMATA. Kwanza anaelezea changamoto wanazokabiliana nazo.
0 COMMENTS:
Post a Comment