Rwanda na Ufaransa jana Jumapili zimekubaliana kurudisha uhusiano wa kidiplomasia, miaka mitatu baada ya Rwanda kuvunja uhusiano.
Makubaliano hayo yalitangazwa na nchi zote. Rwanda ilivunja uhusiano na Ufaransa Novemba mwaka 2006, baada ya jaji mmoja wa uchunguzi wa Ufaransa kumshutumu Rais wa Rwanda Paul Kagame kuamuru mauaji ya mwaka 1994 ya mrithi wake, Juvenal Habyarimana. Ndege ya bwana Habyarimana ilitunguliwa huko Rwanda.
Tukio hilo lilionekana kuchochea mauaji ya halaiki ya Rwanda ambapo waasi wa kihutu waliwauwa watu wapatao laki nane. Katika maendeleo tofauti Rwanda imekubaliwa kujiunga na Jumuia ya Madola. Ni nchi ya 54 kujiunga na kundi hilo ambalo wanachama wengi ni makoloni ya zamani ya Uingereza.
0 COMMENTS:
Post a Comment