Jul 29, 2010

Posted by Dismas Ten in | Thursday, July 29, 2010 No comments

Msosi ni kipengele muhimu sana kwenye maisha ya kila siku ya mwanadamu, na kama kuna wakati ambao huwa unajihisi mzito kutekeleza kipengele hiki basi uko nyuma sana na kamwe hautaweza kwenda na spidi kali ya maisha yaliyojaa sayansi na teknolojia katika ulimwengu huu wa sasa., unajua kwanini? Kama ulikuwa hujui basi sisi tunakujuza hivi ! Sauda Mwilima mtangazaji mahiri wa kipindi cha Bongo Beat kinachoruka kupitia runinga na Staa Tv ni mdau mkubwa wa kufakamia msosi tena ‘Wali na njegere’ yaani mbele ya msosi huo hana muda wa kujiuliza popote anapouana anakandamiza na yuko radhi kukesha akiusubiri kama mpishi atakuwa anasuasua jikoni Upo hapo? “Haki ya Mungu, nauzimia msosi dizaini hiyo kuliko chochote, nikigundua unapikwa niko radhi kukesha kuusubiri na kama jikoni patakuwa panasuasua huwa naamua kwenda huko huko, sikubari mpaka niutie kinywani” alisema Sauda kwa msisitizo

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter