Nov 19, 2009

Posted by Dismas Ten Thursday, November 19, 2009 No comments

Marais Barack Obama wa Marekani na Lee Myung-bak wa Korea ya Kusini wamethibitisha tena nia zao kuhakikisha Korea ya Kaskazini inafutilia mbali mpango wake wa nuklia. Viongozi hao wawili walizungumza na waandishi habari mjini Seoul baada ya kumaliza mazungumzo yao Alhamisi.

Bw Lee alisema, yeye na rais Obama walikubaliana kufanya kazi pamoja kuirudisha Korea ya Kaskazini kwenye mazungumzo ya mataifa sita juu ya mpango wake wa nuklia. Alisema ingawa suala la Korea ya Kaskazini si jambo dogo lakini ushirikiano wa kimataifa kwa wakati huu ni imara.

Bw Obama alihimiza Korea ya Kaskazini kuchukua hatua za dhati kurudi kwenye mazungumzo ya kukomesha mpango wake wa silaha za nuklia. Alisema atampeleka mjumbe maalum wa Marekani Stephen Bosworth hadi Pyongyang mwezi ujao kujaribu kutayarisha duru mpya ya mazungumzo.

Viongozi hao wawili walithibitisha tena umuhimu wa mkataba wa biashara huru kati ya Marekani na Korea Kusini na kuahidi maendeleo yanapatikana kuidhinisha mkataba ambao unahitaji kuidhinishwa na mabunge ya kila nchi, miaka miwili baada ya kutiwa saini.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter