Apr 1, 2010

Posted by Dismas Ten in | Thursday, April 01, 2010 No comments
Mshambuliaji mkongwe wa Nigeria anayechezea klabu ya Portsmouth ya England, Nwanko Kanu bado anasita kukubali ofa ya kwenda kucheza soka nchini Dubai.
Klabu yake ya Portsmouth imepata kibali kutoka kwa wamiliki kuuza wachezaji wake katika kipindi kijacho cha usajili ili kuinusuru timu hiyo kutoka kwenye mzatatizo ya kiuchumi.
Timu ya Al- Ahli ya Dubai ndiyo iliyoonesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa kinigeria mwenye umri wa miaka 33.
Portsmouth iko tayari kumuuza kwa paundi za Uingereza 100,000 na malipo yake katika klabu hiyo ya Dubai yanatarajiwa kuwa paundi 80,000 kwa juma.
Lakini Kanu amesisitiza kuwa hatakimbilia kusaini mkataba huo bali atasubili aone kama kuna timu zingine zitakazoonesha nia ya kumsajili.
Wakati huo huo, meneja wa tottenham, Harry Redknapp amesema kuwa yeye bado ni shabiki mkubwa wa mkongwe huyo wa Nigeria.
Redknapp ndiye aliyemsaidia mchezaji huyo kuwa bora tena katika nafasi yake ya ushambuliaji alipomsajili katika timu Portsmouth wakati yeye akiwa kocha wa timu hiyo ambapo mpaka sasa anamchukulia kama miongoni mwa wachezaji bora aliowahi kuwasajili.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter