Jul 2, 2010

Posted by Dismas Ten in | Friday, July 02, 2010 No comments

King wa Hip Hop na mwana mapinduzi halisi wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo, Joseph Haule a.k.a Professor Jay , mwezi huu anatarajia kufanya ziara kubwa ya muziki nchini Marekani kwa lengo la kuburudisha na kuitangaza zaidi Bongo Fleva kimataifa. Stori za kweli ambazo Jay ‘amelinyetishia’ gazeti hili kuwa atakuwa pande hizo za mzee Obama kwa muda wa majuma kadhaa kuwapa somo (burudani) watoto wa Obama (wananchi wa Marakani) kwa makamuzi anayotarajia kuyafanya kwenye miji kadhaa mikubwa kama Houston – Texas, Boston, na miji mingine kulingana na ratiba atakayopewa baada ya kuwasili huko. “Hii itakua ni ‘tour’ yangu ya kwanza kupiga pande hizo za U.S.A , tangu nilipoanza ‘gemu’ miaka zaidi ya 15 iliyopita, nimejipanga vizuri kuhakikisha nawapagawisha mashabiki wangu wa huko kama ambavyo huwa nafanya hapa bongo na nitahakikisha nagonga ngoma zangu zote kuanzia Chemsha Bongo, Bongo-Dsm, Nikusaidiaje, Zali la mentali, Sauti ya Ghetto, Msilie na zinginezo katika kuhakikisha naipaisha zaidi Bongo Fleva” alisema.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter