Aug 13, 2010

Posted by Dismas Ten in | Friday, August 13, 2010 No comments

MKALI wa miondoko ya Bongo Fleva mwenye maskani yake pande za Tabata Jijini Dar es Salaam Abdul Sykes ' Dully Sykes' a.k.a 'Mr Misifa mzee wa shikide' ameshauriwa kuanza kufanya mazoezi, kupunguza umbo kubwa na kitambi kinachomnyemelea hivi sasa. Mashabiki waliojitokeza ‘Pomoni’ kwenye mpango mzima wa tamasha la Fiesta 'Jipanguse Rraaaaaaaa' lilochukua nafasi pande za viwanja vya Readers Club, jijini Dar walionyesha ‘kushangweka’ vya kutosha pale mchizi alipopanda jukwaani kwa makamuzi, ingawa baada ya muda walianza kumpigia kelele za ‘’wewe punguza kitambi’’ wakimlaumu ‘Mr Misifa’ kwa kuongezeka uzito, kiasi kwamba anashindwa kuonyesha makali yake kama zamani japo alijitahidi kidogo. kwa upande wake Dully alikiri kuogezeka kwa umbo lake na kusema atafanyia kazi ujumbe aliopewa na mashabiki wake huku akiwashukuru mashabiki kwa kumpa sapoti wakati alipokuwa jukuwaani ‘’nawashukuru wale wote waliosema hivyo, naamini hawana nia mbaya kwangu, nitajipanga upya ili kurudisha makali yangu kama zamani " alisema

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter