Oct 27, 2010

Posted by Dismas Ten in | Wednesday, October 27, 2010 No comments
Fernando
Muargentina anayevuna mamilioni Philippines


KATIKA mipangilio ya maisha ya kila siku si ajabu sana kukutana na msemo wa maisha ni popote, ambalo wengi wetu tumekuwa tukiutumia katika kupeana moyo wa kutafuta mafanikio sehemu mbalimbali duniani.

Msemo huu ni moja ya nguzo zinazomgusa nyota anayeshika chati ya juu hivi sasa katika kiwanda cha filamu huko Philippines anayekwenda kwa jina la Fernando.

Akiwa anafanya vizuri kupitia tamthiliya ya "Te Amo, Maging Sino Ka Man" ("I Love You, Whoever You Are") inayong’aa kupitia runinga ya Star TV hapa Bongo nyota huyo anatamba Philippines pamoja na kuzaliwa nchini Argentina.

Katika mazungumzo aliyoyafanya na kituo kimoja cha runinga nchini Mexico, Fernando alieleza kuwa siku zote hatoacha kumshukuru mpenzi wake, Dannay Sengundo ambaye ndiye aliyemshawishi kuingia kwenye fani ya uigizaji.

“Nilipokuwa nakifanya kazi nchini Venezuela, Dannay aliniambia anatamani kama na mimi ningekuwa muigizaji, kwa kuwa nampenda niliamua kulifanyia kazi wazo lake na sasa navuna mamilioni ya pesa kutokana na uigizaji tofauti na kazi niliyokuwa nikiifanya awali,”alisema Fernando.

Maisha ya nyota huyu yalianzia katika mji wa Viedma, Rio Negro nchini Argentina ambako ndiko alikozaliwa na kubatizwa jina la Pedro Cernadas mnamo Machi 20, 1972, ambako pia anajulikana kwa jina la Segundo Cernadas.

Ni mwigizaji wa kiwango cha juu, akiwa amefanya kazi hiyo kwenye mataifa karibuni ya yote yanayounda bara la Amerika Kusini.

Makali ya Fernando katika uigizaji yalianza kuonekana kupitia filamu ya "Ricos y Famosos" ("Rich and Famous"), iliyotikisa Argentina na bara zima la Amerika Kusini kabla ya kwenda kutwaa tuzo ya ‘Major International Hit’ mwaka 1997 nchini Marekeni.

Mwaka 1998, Fernando alitoka na kigongo kingine cha muvi ya "Milady: La Historia Continua" ("Milady: The Story Continues)", ambayo moja kwa moja alimfanya kupata shavu la kufanya kazi nchini Mexico na kuwa mwanzo wa kuikacha nchi yake ya Argentina.

Moto na kasi yake uliitikisa Mexico ambapo siku chache baada ya kutua, alitoa muvi ya "Muñeca brava" ("Wild angel") iliyomfanya kuwa mwigizaji wa kwanza kutoka nje ya nchi hiyo kushinda tuzo ya ‘Major Hit’.

Baada ya mafanikio hayo hatimaye Juni 16, 2000 Fernando alienda Philippines na moja kwa moja akapata nafasi ya kucheza muvi ya kwanza iliyobatizwa jina la "Los Buscas de Siempre" ("The same Bullies of Always)" akitumia jina la "Bebo".


Muvi hii ndiyo ilikuwa mwanzo wa mafanikio na heshima kubwa katika filamu za Philippines, baadaye alitoka na muvi nyingine ya "Los Medicos de Hoy" ("Today's Doctors") akicheza kama daktari, nafasi iliyompa ‘ujiko’ mkubwa na kumfanya kuwa mwigizaji wa kwanza kutoka Argentina kutamba kwenye nchi hiyo inayotajwa kuwa na waigizaji bora duniani hivi sasa.

Kwa wale wanaoikumbuka "Todo Sobre Camila" ("All About Camila") iliyoigizwa nchini Ecuador, watakuwa wamepata mwendelezo mzuri wa kuona moja kati ya filamu zake kali zilizotamba.

Kazi zingine za kijana huyu mtanashati ni pamoja na "Bésame Tonto" ("Kiss me Fool") iliyochezwa kwenye mataifa manne tofauti ya Peru, Dominican Republic, Chile na Panama. Lakini filamu ya "Dr. Amor" ("Dr. Love") iliyotoka mwaka 2003 ndiyo filamu kali na bora kuliko zote alizowahi kucheza akiwa Philippine kwani mpaka leo jina hilo la Dr. Amor ndilo limebaki midomoni mwa wapenzi wengi wa filamu kwa kulichukulia kama jina lake. Unaweza kuitafuta mtaani ili kuthibitisha hilo.

Fernando kwa sasa anang’aa Bongo kupitia Star Tv na tamthiliya ya "Te Amo, Maging Sino Ka Man" ("I Love You, Whoever You Are") akiwa na Iza Calzado ‘Rosela’.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter