Nyota wanaofanya kweli katika kiwanda cha filamu Bongo, Zuena Mohamed ‘Shilole’ na Flora Mvungi ‘The One’ wanatarajia kukwea pipa mapema mwezi ujao kueleka Abuja nchini Nigeria kufuatia mwaliko wa kufanya filamu na dairekta maarufu wa muvi nchini humo Izu Ojukwu.
Wakisema na gazeti hili, juzi kati, ndani ya mjengo wa Hotel ya Lamada Ilala Dar, nyota hao waliofanya kweli kwenye muvi ya ‘Da er Salaaam Sister’ walianika kuwa miezi mitano iliyopita walianza kuwasiliana na dairekta huyo, ikiwa ni pamoja na kumtumia moja ya kazi zao, na sasa mambo yameshaiva kwani amewaita na tayari washakamilisha taratibu za kupata pasi za kusafiria.
“tuko tayari kwa safari ya kwenda kufanya kazi Nollywood mapema mwezi ujao, hizi unazoziona hapa ndiyo pasi zetu za kusafiria”, alisema Shilole huku akionyesha ‘Passport’ yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment