
Wakati Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Dar es Salaam Yanga Afrika wakianza utetezi wa kiti chao kwa sare ya mabao 2-2 na Moro United, Timu ya soka ya Polisi Tanzania imeanza vizuri mzunguko wa pili wa Ligi hiyo kwa kuibamiza JKT Ruvu bao 1-0 katika mchezo mkali uliopigwa kwenye uwanja wa Chamazi Complex uliko Temeke jijini Dar.
Akizungumza na BLOG hii kwa 'shart' la kutokutajwa jina lake mmoja wa viongozi wa timu hiyo amesema kuwa ushindi huo unaifanya timu yake kushika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi huku JKT ikiwa katika nafasi ya 7 na pointi zake17.
"Ni ushindi mzuri umetusogeza hatua moja mbele na kutuondoa kwenye nafasi tuliyokuwa awali tunaka kuendela kushinda pia kwenye michezo inayofuata na hatimaye kuwa kwenye nafasi za juu" alisema kiongozi huyo
 

















 
 
 
0 COMMENTS:
Post a Comment