Jan 16, 2012

Posted by Dismas Ten Monday, January 16, 2012 No comments

Siku moja baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na timu ya Kabuscorp ya Angola ,Kiungo Mshambuliaji Rivaldo Vítor Borba Ferreira wa Brazil amesema Lugha ya Kireno inayotumika Angola ndio iliyomsukuma kutua nchini humo.

Rivaldoliyekuwa akitambulishwa mbele ya vyombo vya habari na kukabidhiwa jezi namba 9 ,amebainisha kuwa alipokea maombi kutoka nchi mbalimbali lakini ameichagua Angola kwa kuwa mradi mzuri uliopo wa kuiendeleza timu Kabuscorp ni sababu nyingine iliyomvuta kwenda Luanda.

Rivardo aliyekuwa hana timu huku akiwa sehemu ya utawala wa timu yake ya Sao Paulo,ameeleza kuwa ameamua kuachana na Sao Paulo kwa vile anajiona ana uwezo wa kuendelea kucheza soka licha ya umri wake kuonekana kumpa kisogo.

Mchezaji huyo anayetumia zaidi guu la Kushoto ametamba kuwa kila nchi anayokwenda kucheza soka mara nyingi huibuka kuwa bingwa jambo ambalo atalifanya kwa Kabuscorp iliyoshika nafasi ya pili ikiwa ni pungufu ya pointi moja tu ya timu iliyotwaa ubingwa.

Amesema ana uhakika atakuwa na furaha na klabu yake hiyo mpya na nchi ya Angola kwa ujumla.

Kabla ya kurudi nyumbani Brazil,Rivaldo aliyetwaa tuzo ya mwanasoka bora wa FIFA mwaka 1999 amewahi kuzichezea timu za AC Milan ya Italia,Olympiakos na AEK Athens.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter