Jul 6, 2012

Posted by Dismas Ten Friday, July 06, 2012 No comments
Uzinduzi wa kampeni kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu ya Yanga unafanyika leo leo katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo makutano ya mitaa Twiga na Jangwani kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Blog hii katibu wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya Yanga Fransis Kaswahili amesema wanataraji kuanza uzinduzi huo saa 10:00 jioni ambapo wagombea wote watakuwepo na kwamba fursa ya kujieleza na kutangaza sera itatolewa kwa wagombea wote.
Kaswahili amesema kikubwa ni kutolewa maelezo ya namna ya kufanya kampeni na utaratibu mzima utakavyo kuwa wakati wote wa kipindi cha kampeni ambazo zitafikia kikomo Julay 14 saa 12:00 jioni.

Aidha amesema kwa ujumla wagombea watatembea matawi takribani 100 ndani ya kipindi hicho huku muda wa kujieleza mbele ya wanachama wa klabu ukiwa ni si zaidi ya dakika tano.
Wakati huo huo kocha mpya wa Yanga Thom Seintfeit anatarajia kuanguka saini ndani ya Klabu hiyo hii katika shughuli ambayo itafanyika pia makao makuu ya klabu hiyo.Taarifa zaidi tuatilia mtandao huu.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter