
MSHAMBULIJI nyota wa klabu ya Barcelona ya Hispania anatarajiwa kuikosa mechi muhimu ya Ligi kuu ya Hispania (La Liga) dhidi ya timu ngumu ya Mallaga kutokana na kuumia kifundo cha mguu wa kulia pia hatakuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo itakapokuwa ikikabiliana ya Dynamo Kiev kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Jumanne ijayo kwenye uwanja wa Now Camp
Taarifa za kitabibu kutoka ndani yaklabu hiyo zinasema kuwa nyota huyo hali yake bado haijaimarika na hatakuwa na uwezo wa kucheza michezo hiyo miwili lakini baada ya mapumziko ya siku 10 anaweza kurejea uwanjani
nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 aliumia kwenye mchezo wa jumanne iliyopita kati ya timu yake na Rancing Santander uliochezwa kwenye uwanja wa El Sardinelo ambapo Barca iliibuka na ushindi wa 4-1 huku mchezaji huyo akifunga bao la kwanza kunako dakika ya 19










0 COMMENTS:
Post a Comment