
Nyota wa klabu ya Man City Emmanuel Adebayor amesema kuwa anataraji kurejea kwa nguvu uwanjani pindi atakapo maliza kutumikia adhabu yake ya kukosa mechi tatu aliyopewa na chama cha soka nchi England FA kufuatia kitendo chake cha kwenda kushangilia bao alilofunga upande walikokuwa wamekaa mashabiki wa Arsenal kitendo kilichotafsriwa kuhatarisha usalama
Adebayor alifanya kituko hicho kwenye mchezo wa ligi kuu ya Backlays mchezo uliomlizika kwa Man City kuibuka na ushindi Mnono wa mabao 4-2 nyota huyo pia alishutumiwa kwa kumchezea rafu mbaya mshambuliaji wa Arsenal ,Robin van Pies.
yaliyotokea yameshapita na niliomba radhi kwa kila aliyetatizika na jambo hilo
ninachokiangalia kwa sasa ni jinsi gani nitaanza kuitumikia klabu yangu kwa nguvu mpya alisema Adebayor wakati azungumza na wanahabari










0 COMMENTS:
Post a Comment