Nov 26, 2009

Posted by Dismas Ten in | Thursday, November 26, 2009 No comments

AZAM FC imetoa wachezaji wanne kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars kinachokwenda Kenya kuwakilisha nchi katika mashindano ya CECAFA Challenge CUP na kuifanya timu ya AZAM FC iwe na wachezaji wengi zaidi kwa timu za Tanzania kufuatia Dan Wagaluka kuwa na Uganda, Vladmir Niyonkuru kuwa na Burundi, Ibrahim Shikanda kuwa na Kenya na Aggrey Morris na Selemani Kassim kuwa na Zanzibar

Hivyo Azam FC imekuwa na wachezaji tisa (9) katika miji ya Nairobi na Mumias. Wachezaji wa Azam FC walio na Kilimanjaro Stars ni Erasto Nyoni, Salum Swedi, Ibrahim Mwaipopo na John Bocco

Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi, Maximo amewajumuisha makipa Shaaban Kado wa Mtibwa Sugar pamoja na Muharami Mohammed aliyetua nchini juzi akitokea Maputo, Msumbiji anakocheza soka ya kulipwa.

Kikosi kamili chini ya mkuu wa msafara ni ambaye ni makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, mbali ya makipa hao ni pamoja na Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Salum Sued, Ibrahim Mwaipopo,Juma Jabu na Shadrack Nsajigwa.

Wengine ni Shaaban Nditi,Nurdin Bakari, David Naftali, Mwinyi Kazimoto, Kigi Makassi,Juma Said 'Nyosso', Henry Joseph (aliyetarajiwa kutua nchini jana usiku), Mussa Hassan Mgosi, Mrisho Ngassa, Jerryson Tegete,Danny Mrwanda na John Bocco.

Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini leo kwa ndege ya Kenya Airways kuelekea Nairobi ikiwa safarini kwenda Mumias ilikopangwa Kundi C kwenye michuano hiyo inayotarajia kuanza Novemba 28 na kuendelea hadi Desemba13.

Michuano hiyo itashirikisha nchi 12 za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na mbili kutoka kusini mwa Afrika ambazo ni Zambia na Zimbabwe ambazo zimealikwa.

Kili Stars ipo Kundi C pamoja na mabingwa watetezi, The Cranes, Uganda, Intamba ya Burundi na Mapinduzi Stars ya Zanzibar .

Akitangaza kikosi hicho jana, Maximo alisema amezingatia mambo kadhaa kuhusu wachezaji hao watakaoiwakilisha nchi kwenye mashindano hayo akiwasihi wawe watulivu, wenye nidhamu na kuweka mbele maslahi ya taifa kama wanahitaji matokeo mazuri.

"Tambueni kuwa mashindano haya ni magumu na yanahitaji umakini mkubwa na muweze kujituma zaidi mnakwenda kukutana na timu ambazo ni ngumu kwa hiyo endepo mtafuata yale niliyowapa na kuzingatia nidhamu ni dhahiri mtafika mbali, "alisema.

Kocha huyo aliongeza kuwa licha ya kuchelewa kwa mlinda mlango Muharami Mohamedi ambaye aliwasili nchini juzi usiku akitokea Msumbiji, bado anaamini kuwa ni kipa bora na mwenye uwezo mzuri kimataifa kwani anafahamu kwa kiasi kikubwa uwezo wake ulivyo.

Akikabidhi bendera ya taifa kwa timu hiyo, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Emmanuel Nchimbi aliwataka wachezaji hao wajitume wakati wote wa mashindano hayo ili warudi na ushindi na kuwaahidi kuwa Watanzania watakuwa nyuma yao wakiwaunga mkono hadi mwisho wa michuano hiyo.

Nahodha wa Kilimanjaro Stars, Salum Sued alisema wamejipanga vizuri ili kurudi na ubingwa mwaka huu kutokana na maandalizi waliyoyafanya chini ya mwalimu wao na kuwataka Watanzania wawaombee ili waweze kufanya vema katika mashindano hayo.

Wadhamini wa timu hiyo, Kampuni ya Bia ya Serengeti wamekabidhi shilingi milion 14 kwa timu hiyo ikiwa ni kwa ajili ya tiketi nza ndege a kuwataka kwenda kufanya vizuri ili kuwapa raha Watanzania

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter