Nov 24, 2009

Posted by Dismas Ten Tuesday, November 24, 2009 No comments




Chama cha Wananchi CUF nchini Tanzania kimesema kimeridhishwa na hotuba ya rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume mbele ya wanachama wa CCM kufuatia mazungumzo yake na kiongozi wa chama hicho Maalim Seif Shariff Hamad.

Mkurugenzi wa wa Idara ya Mambo ya Nje ya CUF Ismail Jussa ameiambia Sauti ya Amerika kuwa kwa ujumla chama chake kimefurahishwa na hotuba ya Rais Karume iliyokuwa na tofauti kubwa na ile ya rais wa awamu iliyopita Dk Salmin Amour.

Amesema jambo la msingi ni kuwa bwana Karume hakutumia maneno ya kejeli kwenye mkutano wake na wananchi wa Zanzibar na badala yake alionesha nia ya kutafuta amani na umoja katika maendeleo na siasa za Zanzibar.

Mkurugenzi huyo pia amesema mgogoro uliokuwepo hapo awali na kupelekea CUF kutomtambua rais Karume na uongozi wake, sasa umekwisha na pande zote ziko tayari kushirikiana.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter