Papa Benedict alitoa ujumbe wake wa Krismasi siku ya Ijuma, saa chache baada ya kuangushwa chini na mwanamke aliyemvamia wakati wa misa ya mkesha ilipoanza katika kanisa la St Peter's Basilica.
Maafisa wa Vatican wameleza kwamba, Papa mwenye umri wa miaka 82 hakujeruhiwa na ratiba yake ya Krismasi iliendelea kama ilivyopangwa. Akizungumza kwa lugha 65 tofauti kutoka baraza kuu ya kanisa, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alisoma dua kwajili ya amani na furaha wakati huu wa sikukuu.
Katika ujumbe wake Papa Benedict, alizungumzia athari za mzozo wa fedha duniani, mizozo huko eneo Takatifu na Afrika, na maafa yanayowapata aliyewataja kundi dogo la wakristo huko Iraq. Alisema mara kwa mara wa kristo wa Irak wanakabiliwa na ghasia na kunyanyaswa.
Kiongozi huyo alitoa ujumbe wake kwa wakati ulopangwa, saa chache baada ya kuvamiwa na mwanamke mwenye umri wa miaka 25. Maafisa wa usalama wa Vatican wanasema yeye ndiye mwanamke yule yule aliyevuka vizuizi na kumkaribia Papa wakati wa misa ya Krismasi mwaka jana.
Hakuna sababu zilizotolewa za mwanamke huyo za kufanya shambulio, lakini maafisa wanasema ni mtu mwenye matatizo ya kiakili. Kardinali wa Kifaransa Roger Etchegaray alijeruhiwa wakati wa tukio hilo.

0 COMMENTS:
Post a Comment