May 8, 2010

Posted by Dismas Ten in | Saturday, May 08, 2010 No comments

haya tena wadau wa blog hii nadhani kila mtu anafahamu kuwa huu ni wakati maalumu wa "Maandalizi kuelekea Afrika Kusini". leo nawamwagia makala mpya kuhusu fainali za kombe la dunia la Afrika Kusini, pia kutakuwa na maelezo kuhusu mustakabali wa timu ya Ufaransa inayoongozwa na Raymond Domenech kwenye fainali za kombe la dunia la Afrika Kusini.

Habari kutoka vyombo vya habari vya Uingereza zinasema, kocha mkuu wa timu ya England Fabio Capello hivi karibuni alitangaza sheria tatu kwa wachezaji wa timu ya England katika kipindi cha fainali za kombe la dunia la Afrika Kusini. Ya kwanza, ni marufuku kwa mchezaji yeyote wa England kutangaza mwenyewe habari kwa vyombo vya habari. Pili, wachezaji hawaruhusiwi kuwasiliana kisirisiri na wachumba au wake zao kwa kutumia mtandao wa internet. Na tatu, wamepigiwa marufuku kukutana na wake zao mara kwa mara. Kwa kuwa katika kipindi cha fainali za kombe la dunia la mwaka 2006, wachezaji wa England walileta matatizo mengi kwa timu hiyo kutokana na kutumia mtandao wa internet mara kwa mara, hivyo Capello alitangaza sheria hizo.

Kocha mkuu wa Ufaransa Raymod Domenech hivi karibuni alisema hawezi kuahidi kuwa Thierry Henry atacheza kwenye kikosi cha timu ya taifa wakati wa fainali za kombe la dunia la Afrika Kusini. Kutokana na kuwa na umri mkubwa na kushuka kwa kiwango cha uchezaji, mshambuliaji wa Ufaransa Henry amekosa nafasi kuu ya kucheza katika klabu ya Barcelona. Kuhusu hilo, Domenech alisema hivi karibuni Henry alicheza mechi chache sana, lakini yeye bado ni mshambuliaji mzuri zaidi kwenye timu ya Ufaransa. Henry alikuwa ni mchezaji hodari zamani na hivi sasa, namheshimu. Lakini siwezi kuahidi kama nitampa nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa, pia anapaswa kugombea nafasi hiyo.

Hivi karibuni mshambuliaji wa Uholanzi Robin Van Persie amepona na kurudi uwanjani, mchezaji huyo alicheza vizuri katika mechi ya ligu kuu ya England. Mwezi Novemba mwaka jana Van Persie alipokuwa akiichezea timu ya Uholanzi alijeruhiwa mifupa ya miguu, hivyo ilimbidi apumzike kwa miezi mitano. Watu wengi walifikiri kuwa atakosa mashindano ya msimu huu hata fainali za kombe la dunia, lakini baada ya kupona aliweza kurudi kwenye timu mwishoni mwa msimu huu. Kutokana na hali yake ya hivi sasa, kuna uwezekano mkubwa kwamba atashiriki kwenye fainali za kombe la dunia.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter