HAKIKA maisha ni safari ndefu , mara nyingine mtu unalazimika kukubali kuwa watu tunatoka mbali nikiwa na maana kuwa mpaka unakuja kuupata utu uzima unakuwa ulishafanya mambo kibao, mazuri kwa mabaya na pia mema na ya hatari du! Kweli acheni Mungu aitwe Mungu.
Lakini leo siandiki makala haya kwa lengo la kukutisha ama kukufanya ulie kwa machungu , bali unaweza kudoNdosha chozi dogo la kishikaji kwa furaha kama ulikuwa mdau wa kweli wa burudani.
Miaka ya 80 hadi miaka ya 90 mpaka 93 ni kipindi ambacho kilikuwa kimechangamka zaidi kiburudani kwani wakati huo ndiyo kilikuwa kinatawala kizazi kipya cha muziki wa Soukouss kutoka huko nchini Zaire (sasa Congo DR) hasa baaada ya kumalizika kwa enzi za akina Luambo Luanzo Makiadi (Franco).
Kabla ya kwenda mbali hebu ngoja nikukumbushe miaka ya karibuni, wanjanja wengi kipindi hicho tulikuwa tunakutana pande za Kinondoni kwenye kiwanja kimoja kilichokuwa na jina la Tazara Hostel.
Hapo ‘baba’ kulikuwa kunapigwa ngoma na bolingo za kufa mtu hakuna kulala mpaka kunakucha ni mwendo wa ‘Soukouss’ kwa kwenda mbele chini ya DJ maarufu ‘Le Generali’ Charles Mhamiji.
Lakini leo hii maeneo hayo yako kimyaa! hakuna bolingo wala disco watu wanapiga usingizi tu kwenye majengo hayo baada ya kubadilishwa na kuwa Hostel.
Hapo nadhani nimekugusa kidogo, sasa mpango mzima uko hivi, kwa wewe uliyependa burudani ya muziki wa Kiafrika hasahasa kutoka pande hizo za Zaire nadhani unakumbuka enzi hiyo ambayo tulikuwa tunaalikana kwa maneno ya ‘’Ebwana leo vipi leo hatuendi Buggy’’ halafu utasikia mtu anajibu ‘’wewe tusiende nani kasema’’na hatimaye mida fulani ya jioni tuajisogea pande hizo za Tazara Hostel kusongesha Buggy lenyewe.
Hakika ilikuwa utamu kolea lakini sasa burudani hiyo haipo tena hapa bongo kilichopo ni mlolongo wa shoo za wana bongo fleva huku bendi zinazopiga muziki staili hiyo kama Akudo na FM Academia taratibu zinaanza kukosa wadau.
Sina hakika sana pengine hii inachangiwa na nini? Labda kupanda kwa gharama za maisha, au kukosekana kwa wanamuziki nyota kama waliokuwepo enzi hizo.
Kila mpenda ‘Buggy anakumbuka ngoma kali zilizokuwa zinapigwa na wakali kutoka kundi la Loketo Group, hivi ni nani aliyekaa kwenye kiti wakati ngoma kama ‘Evelina, ama ‘Huke loketo’ zikiwa hewani chini ya DJ Charles.
Utamu wa sauti kutoka kwa Lucian Bokilo na utundu wa kucharaza gitaa wa Dally Kimoko ulitosha kabisa kuwapagawisha watu mpaka wanasahau kama kuna kesho.
Lakini leo hii hakuna vitu adimu ama hivyo baba zaidi ya kusikia ‘yoyoo’na pedeshee fulani halafu muziki wenyewe umedoodaa da! Hii inaniuma sasa nani leo anaweza kutufuta chozi la kukosa vitu hivyo adimu.
Hebu kumbuka hii wakati unendelea kuburudika na Loketo ya Aurus Mabele iliyokuwa inanogeshwa na akina Lokasa ya Mbongo, ghafla anapandishwa hewani ‘Mzee Benz’ Bozi Boziana, na kwa mbaali unaisika sauti ya mwanadada Scola Miel wakilisukuma Nzawisa, mama Nzawisa , jamani ilikuwa ni nusu kupata uchizi,
Wakati unapagwa na ngoma za ‘Soukouss’ hapo hapo kichwani kuna Pilsner kama saba hivi wewee acha kabisa lakini bia hiyo leo haipo tena baba du !!!!!!!!!!!
Kali zaidi mida fulani ya saa nane nane wakati watu mshaanza kuchoka anapandishwa hewani ‘’Mzee wa Fujo’’ Alan Kounkou hapo hata waliojificha kwenye kona wanaibuka na baada ya sekunde kadhaa Jean Baron anaingia na songi lake ‘Mami lolo’ du! Hakika ni balaa kutoka unataka, kubaki unataka, basi unajikuta upo kati ukiendelea kusukuma Buggy mpaka busheee.
Wajanja wengi tulikuwa tunajua kuwa ukiona ngoma zinapungua kasi na kuanza kupigwa za akina Solomon ‘Rama rama’ au ‘Double Double’ ya Nyboma ujue asubuhi iko karibu basi hapo tunaitana na kukata maji ya mwisho mwisho na kuchukua totoz zetu halafu haooooo ‘mahome’
Barabarani tunakutana na ndata (Polisi) kibao wakiwa wanajiwahisha sehemu zao za kazi lakini kwa kuwa tuko matingas (ulevi kupindukia) tunaanchana nao.
Halafu kesho yake Jumapili haooo tunaenda zetu uwanja wa Taifa, kucheki bonge la mechi la watoto wa mjini Nyota Nyekundu na Sigara. Upo hapo? Na wikiend inakuwa imekamilika SAAAAAAFI.
Jamani nimeandika hii kukumbukia enzi kidogo, kwani leo hii mambo hayo hakuna tenam Najua sijataja kila kitu lakini Mungu awalalaze pema marehemu Kabasele Yampanya ‘Pepe Kale’ Madilu Systeme na wengine kwani ngoma zao zilitupagawisha mno enzi hizo.

0 COMMENTS:
Post a Comment