MCHEZA sinema maarufu Mel Gibson amedaiwa kutaka kumpa mzazi mwenziye, Oksana, dola milioni 20 ili aweze kushiriki matunzo ya mtoto wao mchanga kwa pamoja. Hata hivyo, mwanamke huyo amezikataa fedha hizo kutokana na tabia ya ukorofi aliyo nayo Gibson, hivyo kuona mtoto wake hafai kuishi karibu na jamaa huyo. Kwa mujibu wa mtandao wa RadarOnline, siri hiyo ilifichuka baada ya kanda ya siri kumwonyesha Mel akimrushia Oksana matusi ya kibaguzi na kijinsia, jambo ambalo lilizima kabisa jaribio la ‘kumhonga’ mzazi mwenziye fedha hizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment