IWAPO kutoa msamaha ni jambo la utukufu wa mbinguni, basi mwanamuziki wa kike wa Marekani, Rihanna, anaelekea kuukwaa utakatifu.
Jarida la ‘Heat Magazine’ kwa kupitia mtandano wa MTV wa Uingereza, limeripoti kwamba mwanamuziki huyo anayetamba kwa kibao chake cha “Rude Boy” anataka kurejesha uhusiano wake na kipenzi chake wa zamani wa kiume, Chris Brown, ambaye alimshambulia kwa kumtwanga vibaya baada ya hafla ya tuzo za Grammy mwaka jana.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja, Rihanna ameongea na Brown kwa simu na kutaka kurudisha uhusiano wao baada ya hivi karibuni kimwana huyo kuonana na mpenzi wake huyo wa zamani na kugundua bado ana uchu wa kulirudisha penzi lao.
Hivi sasa Rihanna anajivinjari na Matt Kemp, nyota wa mchezo wa mpira wa kikapu wa timu ya Los Angeles Dodgers.
0 COMMENTS:
Post a Comment