Aug 2, 2010

Posted by Dismas Ten in | Monday, August 02, 2010 No comments
Hapana shaka kuwa mashabiki wa burudani waliohudhuria tamasha kubwa la muziki lijulikanalo kama ‘Fiesta Jipanguse’ lilochukua nafasi ndani ya Uwanja wa Jamhuri pande za ‘mji kasoro Bahari’ (Morogoro) watakuwa wanamkumbuka vizuri nyota aliyefunika asilimia mia moja kwenye ‘shoo’ hiyo, Ibrahim Gunda Shani a.k.a ‘G-One’ Dodoso za gazeti hili zimebaini kuwa mkali huyo aliyewapagawisha mashabiki siku ya tamasha hilo kwa wimbo wake maarufu wa ‘Mrembo wa kiafrika’ ni Mganga wa jadi na hivi sasa ameamua kuyapa kisogo makazi yake ya awali mjini Morogoro na kuhamia Tandale ndani ya Jiji la Mh. Lukuvi (Dar Es Salaam) Akistorisha ‘Laivu’ na gazeti hili hivi karibuni G -0ne aliweka wazi kuwa alianza kujihusisha na masuala ya ukalumanzila mwaka 1999 mara baada ya kuhitimu Kidato cha Nne kwenye Shule ya Sekondari, ‘Moro Sec’ licha ya kuwa wakati huo alikuwa akijihusisha na muziki. “Nikiwa bado niko shule nilikuwa nafuatilia tiba za jadi kwa wazee na watu wangu wa karibu waliokuwa wanjihusisha nazo , nilipomaliza kidato cha nne nilichukuliwa na maruhani hadi porini ambako nilifundishwa njia mbalimbali za kutibu kwa mwaka mmoja na nusu huku ndugu zangu wakiamini kuwa nilipotea,” alisema G-One. Aidha, nyota huyo aliendelea kusema baada ya kumaliza mafunzo hayo aliyokuwa anapewa na watu wasioonekana huku akiishi kwa kula mizizi, bila kujua alijikuta yupo katikati ya Mji wa Morogoro huku akiwa na ujumbe uliomtaka kuendelea na kazi hiyo. Hata hivyo G- aliweka wazi kuwa anaifanya kazi hiyo kwa kuwa anaipenda pia ni sehemu ya maisha ya mwanadamu kufanya vitu au kazi tofauti ndiyo maana ameiweka mbele licha ya kuwa ana kipaji cha muziki. Kuhusu muziki, G-one alitanabaisha kuwa uko kwenye damu na baada ya kupiga ‘shoo’ bora kwenye tamasha la ‘fiesta’ yuko tayari kuachia mtaani albamu yake aliyoibatiza jina la ngoma iliyompaisha ya ‘Mrembo wa Kiafrika’ na tayari ameshaachia hewani video ya ngoma hiyo.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter