Aug 2, 2010

Posted by Dismas Ten in | Monday, August 02, 2010 No comments

Nyota mwenye mafanikio katika tasnia ya filamu hapa nchini, Blandina Chagula a.k.a Johari, mwishoni mwa wiki iliyopita alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akimwaga chozi mbele ya kundi la watoto waliomtembelea nyumbani kwao mjini Shinyanga.

Johari aliyekuwa Shinyanga kwa mapumziko ya wiki moja, alitanabaisha kuwa alikuwa kwenye wakati mgumu baada ya watoto hao kuanza kumsimulia ‘masaibu’ yao huku wakilia na kumuomba msaada wa kuwasomesha kufuatia kutelekezwa na wazazi wao na kujikuta wakiishi maisha ya mitaani.

“Maneno yao yalikuwa na ujumbe mzito wenye huzuni na uchungu mkubwa, hakika niliingiwa na uchungu na kujikuta nikimwaga chozi mbele yao, hata hivyo nimewaahidi kuwatafutia njia ya kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kuzungumza na Jumuiya ya Wazazi ya Mkoa wa Shinyanga” alisema Johari.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter