
Tukio hilo lililoshuhudiwa ‘live’ na safu hii lilianza kwa nyota huyo kuaga kwa watu wake kuwa anaingia kidogo ‘kuchimba dawa,’ na wakati akiendelea na mpango wake huo ndipo zoezi la kulipua fataki za kusherehesha shoo hiyo iliyochukua nafasi Viwanja vya Leaders Club lilipoanza kufanyika na kumfanya staa huyo atoke ‘chimbo’ mkuku kwa hofu.
“Nimeshtuka kidogo ndugu yangu, nilikuwa sijui nini kinaendelea duh! Yaani ghafla nimehisi usalama umepotea ndiyo maana nimetoka chimbo mkuku,” alisema Diamond huku akiungana na washikaji waliokuwa karibu kuzimia kwa kicheko
0 COMMENTS:
Post a Comment