KIONGOZI wa kundi mahiri la Tip Top Connection linalotamba kwenye ‘gemu’ ya Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’ amesema licha ya kufunika kwa ‘viwalo vikali’ kundi hilo lilipanga kutumia helikopta kuingia kwenye viwanja vya ‘Leaders Club’ ambako mpango mzima wa Fiesta 2010 Jipanguse Rraaaaaa ulikuwa unakamilika
Akichonga na Fleva mchanganyiko ‘Bakisteji’ muda mfupi baada ya funiko la shoo ya kimataifa jukwaani ‘Madee’ alisema watu wengi wamekuwa ‘saplaizid’ na sisi kugonga ‘suti’ lakini mpango wetu kabla ulikuwa ni kuingia kwa helikopta uwanjani hapo lakini serikali ikatuzuia kwa sababu za kiusalama.
“Tulitaka kuwaonyesha watu uwezo wa kundi letu kifedha kwa kudondoka na helikopta lakini serikali ikazima ndoto zetu, hata hivyo pigo la suti zaidi ya kumi zenye thamani ya shilingi milionI moja na ushee limewakimbiza watu,” alisema Madee kwa kujigamba.
0 COMMENTS:
Post a Comment