Ni miaka zaidi ya 20 sasa tangu kuingia na kukubalika kwa Muziki wa Kizazi kipya katika jamii ya Watanzania ambao asilimia kubwa ni wadau wakubwa wa burudani. Lakini pamoja na kuwa na muda murefu katika ‘gemu’ wasanii wa muziki huo wamekuwa na kilio cha miaka nenda rudi juu ya malipo kidogo wanayopata kutokana na kazi zao na zaidi haijulikani kama kuna anayesikia kilio hicho. Hakika kilio hiki ambacho sana kinaelekezwa kwa wasambazaji wa kazi hizo kimekuwa kama ‘donda ndungu’ ambalo halisikii dawa japokuwa jitihada za kulikomesha huwa zinafanyika kila siku Huwezi kuamini kuwa mpaka leo msanii anapata shilingi 50 au 30 ya malipo kutoka kwenye kila ‘tepu’ moja inayouzwa dukani pindi anapokuwa ametoa albamu na kiasi kilichobaki anafaidi msambazaji Ni wazi kuwa kunahitajika jitihada za makusudi kuwaokowa wasanii wetu na janga hili, ili angalau maisha yao yaweze kubadilika na kufanana na hadhi waliyonayo kwani bila hivyo kilio chao kitakuwa sawa na kilio cha samaki ambacho tunaambiwa hakina machozi wakati ukweli ni kuwa machozi yake yamekwenda na maji
Aug 13, 2010

TAFUTA HAPA
HABARI MUHIMU
-
Namshukuru Mungu kwa kunipa uhai mpaka simu ya leo na kunifanya nipate kuongea nawe msomaji kwa njia hii ya safu ya mkasa wa simu. Kwa jina ...
-
Katika hali ya kushangaza, mapema wiki hii Mwanamitindo mahiri nchini Ureno, Nereida Gallardo amewaambia waandishi wa habari kuw...
-
Mwanamitindo maarufu nchini Marekani Christine Mendoza amesema ameandaa mpango maalumu wa kumnasa kimapenzi nahodha wa wa zamani...
0 COMMENTS:
Post a Comment