Dec 23, 2010

Posted by Dismas Ten Thursday, December 23, 2010 1 comment
FLORA MVUNGI 'THE ONE'

Diva wa kiwanda cha filamu Bongo, Flora Mvungi amesema ameamua ‘kuipa kisogo’ kwa muda kambi hiyo na kujiunga na ‘gemu’ ya muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’


Akisema na www.dismasten.blogspot.com ‘juzi kati’ ndani ya hotel ya Atriums pande za Sinza jijini Dar, nyota huyo wa filamu ya ‘Domestic Love’ alitanabaisha kuwa tangu kitambo alikuwa na ndoto ya kufanya muziki wa kizazi kipya lakini ratiba ndefu ya kazi za filamu imekuwa ikimnyima uhuru ndiyo maana sasa ameamua kuachana nayo na kugeukia Bongo Fleva.


“Unajua toka zamani nilikuwa na hamu ya kufanaya muziki lakini ratiba za filamu zilininyima uhuru ndiyo maana sasa nimeamua kuziweka kando, na hivi ninavyoongea na wewe tayari nimeshamamaliza kurekodi nwimbo wangu wa kwanza pale ‘Shalobaro Rec’ kwa Bob Junior” alisema Flora bila kutaja jina la wimbo huo

1 COMMENTS:

Anonymous said...

huna lolote tunakujuwa

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter