Dec 23, 2010

Posted by Dismas Ten in | Thursday, December 23, 2010 No comments
STEVEN CHARLES KANUMBA

I con wa kiwanda cha filamu Bongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’ amegoma kuyaanika hadharani mapato yanayopatika ktokanana uuzwaji wa filamu zinazotolewa na wasanii wanaondaa muvi nchini.

Akizungumza na www.dismasten.blogspot.com, mapema jana Kanumba aneyafanya vizuri sokoni na filamu yake ya ‘More Than Pain’ alisema licha ya kukua kwa tasnia ya filamu hapa nchini lakini suala la mapato yanayopatika baada ya filamu kuingizwa sokoni yanabaki kuwa siri ya mtayarishaji au watayarishaji wa filamu husika.

“Ni kweli kuwa tasnia ya filamu hivi sasa inakuwa hii ikiwa na maana kuwa wadau wetu, wameikubari na wananunua kazi zetu lakini suala la kiasi gani kinapatikana kwa mauzo ya filamu moja itabaki kuwa siri ya watayarishaji husika na kamwe siwezi kuisema hapa” alisema Kanumba.

Alipoulizwa kama uwoga huo wa kutaja mapato unatokana na kuogopa makali ya serikali Kanumba alisema hana uhakika juu ya hilo lakini anachokifahamu ni kuwa mapato bado yataendelea kubaki siri ya watayarishaji, mpaka hapo baadae hali itakapokuwa nzuri zaidi.

Sina hakika kama kuna mtu anawea kukwepa mkono wa serikali, lakini kwa sasa bado itaendelea kuwa hivyo mpaka hapo baadae mambo yatakapokuwa mazuri zaidi ndiyo tunaweza kutaja kiwango kinachopatikana alisema Kanumba.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter