Dec 23, 2010

Posted by Dismas Ten in | Thursday, December 23, 2010 No comments
SEIF SHAABAN 'MATONYA'

Nyota wa Muziki wa kizazi kipya Bongo, Seif Shaban ‘Matonya’ mwenye maskani yake pande za Tanga, ameibuka na kutupilia mbali tetesi kuwa ukimywa wake kwenye ‘gemu’ hivi sasa unatokana kuishiwa mashairi jambo linalomfanya kushindwa kutunga ngoma zenye kiwango kama alivyokuwa akifanya hapo awali.

Akizungumza na www.dismasten.blogspot , juzi kati pande za My fair jijini Dar Matonya aliyewahi kuitikisasa Bongo kwa ngoma ya ‘Vailetti’alifunguka kuwa kumekuwa na tetesi kitaa kuwa ameishiwa mashari na hawezi tena kufanya vizuri kwenye muziki kama alivyokuwa mwazo kwa kuwa sehemu kubwa ya nyimbo zilizokuwa zinampa chati wakati huo alikuwa akitungiwa na watu.

“Kaka mimi sijafulia kimawazo, bali ukimya wangu hivi sasa ni mikakati tu ya kujiweka sawa na mabadailliko ya muziki wetu unaoendelea kukua kila siku, kumbuka hivi sasa muziki ndiyo kila kitu kwenye maisha yangu kwa hiyo siwezi kufanya kazi kwa kukurupuka, nataka kufanya kazi kwa mpango na kusaka mafanikio kwenye levo za kimataifa zaidi” alisema Matonya ambaye pia ndiyo mtunzi wa kibao matata cha ‘Anita’.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter