Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Athumani Mwingereza ‘Tanzanite’ aliyeibukia mlango wa nyuma baada ya ‘kukopi na kupesti’ wimbo wa ‘Mbagala’ ulioimbwa na mkali Nasib Abdul ‘Diamond’ ameiacha kwenye mataa lebo iliyomtoa ya Matunguli Fleva na kutimkia Dhahabu Record inayoongozwa na ‘Handsome’ Abdul Abby Sykes ‘Dully Sykes’.
Akizungumza na www.dismasten.blogspot, Tanzanite alitanabaisha kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo ikiwa ni mpango mmoja wapo wa kujiimarisha na kukuza kiwango chake cha muziki na pia kujiweka tayari kwa ujio wake mpya kwenye ‘gemu’ hiyo.
“Nimeamua kujiunga na Dhahabu Record ili kujiimarisha zaidi kimuziki huku pia lengo langu ikiwa ni kuweka sawa ujio wa kazi yangu mpya ambayo haitategemea mgongo wa mtu mwingine kama ambayo nilifanya kwenye wimbo wa ‘Kafara’” alisema Tanzanite
0 COMMENTS:
Post a Comment