Mabao yaliyofungwa na wachezaji Haruna Moshi na Gervas Kago katika mpambano dhidi ya Coastal Union yameiwezesha timu ya Simba kuendelea kujiimarisha kileleni katika msimamo wa ligi kuu baada ya kufikisha point 31.Mchezo huo wa ligi kuu uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dsm Wekundu hao wa Msimbazi walikuwa kwanza kupata baohiloambalo lilidumu hadi ngwe ya kwanza inamalizika.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Simba waliongeza bao la pili kabla ya wagosi wa Kaya kupata bao ka njia ya tuta lililofungwa na Hamis Shengo.
Timu ya Coastal Union ambayo ilikuwa na kila ya sababu ya kulipiza kisasi baada ya mchezo wa mzunguko wa kwanza kuchapa nyumbani mabao 2-0 kwa matokeo hayo imeendelea kujiweka katika hatari ya kuporoka daraja ikibaki na pointi 11 nafasi ya kumi na tatu.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo timu ya Azam FC wakiwa nyumbani Chamanzi wamechimza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon,John Boko akifunga la kwanza kabla la pili kujifunga wenyewe na lile laLyon likifungwa na Sammy Kessy.
Azam Fc sasa imefikisha pointi 25 ikiwa nafasi ya nne nyuma ya Oljoro waliyopishana kwa pointi moja.










0 COMMENTS:
Post a Comment