Jan 30, 2012

Posted by Dismas Ten Monday, January 30, 2012 No comments
Kufuatia ushindi wa mabao 3-1 iliyoupata juma lilipita dhidi ya Jkt Ruvu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mabingwa wa soka nchini Young Africans Sports Club wametamba kuibuka na ushindi katika michezo yao yote inayofuata.

Akizungumza na Blog hii, Msemaji wa klabu hiyo Louis Sendeu amesema kuwa uimara wa kikosi chake hivi sasa unampa uhakika wa kushinda michezo yote inayofuata kwenye mzunguko wa pili wa ligi hiyo ukiwemo ule wa watani zao wa jadi Simba Sc ya jijini.

"Kwa sasa kikosi chetu kipo katika hali nzuri, tunaimani kubwa na kocha wetu Papic hasa wakati huu wa kuelekea mchezo wa klabu bingwa ya Afrika dhidi ya Zamalek ya Misri na tunauhakika wa kushinda michezo yetu yote iliyosalia kwenye mzunguko huu wa pili ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Simba" alisema Sendeu.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter