Katika hali isiyo ya kawaida hasa baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya timu ya Taifa ya wanawake ya Namibia, wadau wa soka nchini wameimwagia sifa kemkem timu ya Taifa soka ya wanawake Twiga Stars.wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao wamesema kuwa hivi sasa kuna haja kubwa kwa shirikisho la kandanda nchini TFF kuipa kipaumbele kikubwa timu hii ili kuiwezesha kuwa na mafanikio zaidi.
'Hakika wameonyesha kuwa wanaweza kwani walichokifanya kila mmoja amekiona, ni wakati sasa kwa TFF kutoa kipaumbele kikubwa kwa timu hii ili kusuma kufika juu zaidi ya hapo" alisema Mkuu wilaya ya Bahi mkoni Dodoma Betty Mkwasa.
Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh Idd Azzan ambaye pia ndiye mmoja wa asisi wa timu hiyo ameitaka TFF kuiimarisha ligi ya Wanake ili kuweza kupata wachezaji wazuri zaidi watakaofaa kuitumikia Twiga Star siku za Usoni.










0 COMMENTS:
Post a Comment