Wakati tarehe ya mwisho kwa vilabu vya ligi kuu kutangaza wachezaji wao itakao waacha ikiwa inaelekea ukingoni june 31 2012, klabu ya Yanga hii leo imetangaza kuwaacha jumla ya wachezaji 10.
Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na wachezaji wawili raia wa kigeni Davis Mwape raia wa Zambia na Kenneth Asamoah raia wa Ghana.
Asamoah ameachwa na Yanga baada ya klabu hiyo kuvunja mkataba wake ambao ulikuwa umebakia mwaka mmoja.
Wengine walioachwa ni pamoja na ndugu wawili Abuu Ubwa na Zuberi Ubwa ambao hawakuwa na msimu mzuri katika msimu uliopita ndani ya klabu hiyo.
Wachezaji wengine ni Godfrey Born , Julias Mrope , Iddi Mbaga , Atif Amour na Kiggi Mkasi.
Msemaji wa Yanga Luis Sendeu amesema kuwa mlinda mlango Shabani Kado aliyejiunga na Yanga akitokea timu ya Mtibwa sasa anarejea katika timu kwa mkopo.
Katika usajili wake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na michuano ya kombe la Kagame Yanga imewasajili wachezaji kadhaa akiwemo
Kelvin Yondani Ally Mustafa Bartez toka Simba, Frank Dumayo toka JKT Ruvu,Nizar Khalfani huru akitokea nchini Marekani ,Ladslaus Mbogo toka Toto Afrika ya Mwanza na Simon Msuva toka Moro United.
0 COMMENTS:
Post a Comment