Jun 21, 2012

Posted by Dismas Ten Thursday, June 21, 2012 No comments

Ngasa enzi za Yanga
Baada ya kuitumikia klabu yake ya Azam kwa msimu wa 2010/2011 pamoja msimu wa 2011/2012 hatimaye kiungo hodari wa pembeni Mrisho Khalfani Ngasa sasa anarejea katika klabu yake ya zamani ya Yanga wakati akiwa bado kumalizia mwaka mmoja  mkataba wake na klabu yake anayochezea sasa ya Azam.
 Mrisho Ngasa ambaye ameeendelea kulinda kiwango chake katika muda wote akiwa na Azam amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu kutaka kurejea Jangwani ambako anaonekana amekuwa na mahaba nako.
Taarifa  zinasema kuwa kiungo huyo asubuhi ya leo alionekana katika makao makuu ya klabu ya Yanga na kuelekea moja kwa moja katika ofisi ya katibu makuu wa klabu hiyo ambako walikuwemo viongozi wa Yanga John Celestine Mwesigwa na baadhi ya wanachama waandamizi kama Seif Magari ambaye ni msimamizi mkuu wa usajili wa Yanga.
Mrisho Ngasa
Taarifa  zinasema kuwa Yanga inampango wa kuvunja mkataba wa Ngasa katika klabu yake ya Azam ambao umesali mwaka mmoja kama ilivyokuwa kwa Azam ambayo ilifanya hivyo mwaka 2010 wakati wa usajili.
Ngasa leo alionekana akiranda ndani ya makao makuu ya klabu hiyo akionekana kama mwenyeji na kuingia katika vyumba vya wachezaji na baadhi ya wanachama na wapenzi waliokuwepo klabu asubuhi ya leo walionekana kumpokea kwa kumshangilia na kumuonyesha bashasha kubwa muda wote tangu akiingia na wakati akiondoka.
Ngasa akiwa katika majukumu ya kitaifa
Azam ilitumia kiasi cha shilingi milioni tisini kumsajili Ngasa ikiwa ni pamoja na ada ya uhamisho wa usajili wake. Swali,  Yanga itatumia kiasi gani kufanikisha hilo? tusubiri.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter