Jun 21, 2012

Posted by Dismas Ten Thursday, June 21, 2012 No comments

Emmanuel Okwi
Mabingwa wakandanda wa ligi kuu ya nchini Afrika kusini  Orlando Pirates imeonysha nia ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi.
Okwi ambaye kwasasa anatoa huduma katika klabu ya simba alikuwa katika kiwango cha juu katika ligi kuu ya Tanzania Bara “Vodacom Premier League” na akifanikiwa kufunga goli katika mchezo wa kimataifa wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya Angola mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 huko katika mji wa Luanda nchini Angola.
Mwishoni mwa juma nchini Uganda Okwi alikuwa ni miongoni mwa wafunga ji wa mabao ya ushindi 4-0 dhidi ya Congo.
Msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga amethibisha kuwa mabingwa hao watetezi wa ligi ya Afrika kusini wanamtaka mshambuliaji huyo wa zamani wa Sports Club Vill.
Emmanuel Okwi akiwa katika mazoezi na timu yake ya taifa ya Uganda The Cranes
Kamwaga amekaririwa akisema
“Orlando Pirates wanataka kumsajili wamemualika kwa majaribio ya wiki tatu na wataamua endapo watataka ajiunge nao.”
“tunamsubiri Okwi arejee kutoka Uganda ambako alikuwa akiitumikia timu yake ya taifa na ataamua kama atataka kwenda kujaribu.”
Kamwaga akaendelea kusema kuwa katika michezo kadhaa ya kujenga kikosi cha Orlando Pirates atajumuishwa.
“moja kati ya mechi atakazo cheza ni dhidi ya Newcastle United ambayo itakuwa ziarani na itacheza na Orlando Pirates.”
Kama ataondoka katika ligi yake ya sasa ya Vodacom Premier League na kujiunga na ligi ya Afrika kusini PSL champions, huu utakuwa ni usajili wa kuvunja rikodi katika soka la Tanzanian.

0 COMMENTS:

TAFUTA HAPA

UNGANA NASI

Delicious Digg Facebook Favorites More Stumbleupon Twitter