Kiungo
mahiri wa klabu ya Yanga Haruna Niyonzima aliyoko nchini Rwanda
alikokuwa aanakitumikia kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda katika
michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia 2014 nchini
Brazil na pia fainali za mataifa ya mwaka 2013 nchini Afrika kusini
anatarajiwa kurejea nchini ndani ya siku mbili zijazo kujiunga na
wachezaji wenzake wa Yanga kwa ajili ya maandalizi ya kombe la Kagame
ujao.
Haruna ambaye ni
kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Yanga amefanya mazungumzo na Blog hii na kusema kuwa amemaliza majukumu yake ya kitaifa nchini
Rwanda na anajipanga kurejea nchini ndani ya siku mbili zijazo tayari
kutoa huduma yake ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake katika makutano
ya mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Niyonzima amesema
amefurahishwa na usajili unaoendelea katika klabu yake huku akisema ana
imani na wachezaji wapya wanaosajiliwa na klabu kwasasa na kwamba uwezo
wa kiungo wa pembeni wa Nizar Khalfani anaufahamu na anadhani Yanga sasa
itakuwa na viungo imara watakao unganisha kikosi katika michezo
mbalimbali.
hata hivyo amekanusha taarifa za hivi
karibuni kuwa alikuwa akifanya kazi ya kuisaidia Yanga kusaka wachezaji
toka Rwanda isipokuwa aliwahi kushawishi Yanga kuwasajili baadhi ya
wachezaji ambao hata hivyo hakutaka kuwataja majina yao ambapo klabu
ilimuahidi kuyashughulikia maoni yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment