Kamati
ya usajili ya klabu yanga inayoongozwa na Salum Rupia kwa kushirikiana
na kamati ya usajili sambamba na Benchi la ufundi la klabu hiyo,
imejikuta katika wakati mgumu kufuatia wachezaji wake kadhaa wanaotakiwa
kuondolewa katika orodha ya wachezaji wa klabu hiyo kwa ajili ya msimu
ujao ligi kugomea hatua hiyo ya kuondoka ilhali bado wanamikataba ndabni
ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani toka kwa
mtu wa karibu na kamati hiyo ni mwamba mchezaji raia wa Ghana
aliyesajiliwa na klabu hiyo kongwe barani mwaka 2010 kwa mbwembwe
Kenneth Asamoah amegomea kukatishiwa mkataba wake kwa kile
kilichoonekana kushindwa kuafikiana kwa baadhi ya mambo likiwemo suala
zima la malipo ya kuukata mkataba huo ambao umesalia mwaka mmoja
kumalizika.
Wachezaji wengine ambao nao wanatakiwa
kupunguzwa na kupisha nafasi kwa wachezaji wengine ambao wanahitajika
msimu huu ni Pamoja na Julias Mrope na Pius Kasambale ambao wote
waliitwa na kamati ya usajili ya Yanga jana kuelezwa juu ya azma ya
klabu hiyo kuwatafutia timu nyingine ambazo wataelekea huko kwa mkopo
wameonekana kuchachamaa na kupinga hatua hiyo ya kamati ya usajili ya
Yanga.
Hatua hiyo imezua utata na hali ya
sintofahamu wakati huu ambapo shirikisho la soka nchini Tanzania TFF
limetangaza kuongeza muda wa tarehe ya mwisho ya kutangaza wachezaji
watakao achwa na vilabu mbalimbali huku vigogo Simba na Yanga kama
kawaida yao wakiendelea kusuasua kufanya hivyo.
Wakati dirisha la usajili likitarajiwa
kufungwa tarehe 30/06/2012 Yanga tayari imesha kamilisha usajili wa
wachezaji kadhaa akiwemo Kelvin Yondani toka Simba, Frank Domayo toka
JKT Ruvu, Nizar Khalfani mchezaji huru aliyekuwa akichezea soka katika
klabu Vancouver White Caps ya Canada na Ally Mustaafa "Bartez" toka
Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment